Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muungano wa posta kuweka viwango vya usalama:UPU

Muungano wa posta kuweka viwango vya usalama:UPU

Kamati mpya ya masuala ya usalama ya muungano wa kimataifa wa Posta UPU, waendesha huduma za posta na mashirika ya kimataifa wamekutana kwa mara ya kwanza kwenye makao makuu ya UPU kujadili masuala mya usalama wa posta.

Wadau hao wamejadili maendeleo na kutumia viwango vya kimataifa vya usalama ili kuboresha usalama katika usambazaji wa kimataifa. Mkurugenzi mkuu wa UPU Edouard Dayan amesema ni muhimu kushirikiana katika kiwango cha kimataifa kuweka viwango vinavyohitajika vya usalama kwa wote kuliko kila nchi peke yake.

Mkutano huo unafuatia hatua za mwaka jana zilizochukuliwa na Marekani baada ya vifurushi viwili vilivyokuwa na mabomu kutoka Yemen kubainika. George Njogopa anaarifu.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)