Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi za kimataifa zinahitajika kukabili uharamia:Ban

Juhudi za kimataifa zinahitajika kukabili uharamia:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ametoa wito wa kuwepo na juhudi za kina kupambana na uharamia kwenye pwani ya Somalia, akisema hali hiyo ni matokeo ya ukosefu wa usalama, kutokuwepo na serikali imara na umasikini kwenye taifa hilo la pembe ya Afrika.

Ban amesema uharamia sio maradhi yatokanayo na maji, bali ni dalili ya hali halisi kwenye eneo hilo ambayo inajumuisha usalama na matatizo ya kisiasa Somalia.

Ban ametuma ujumbe huo kwenye mkutano kuhusu uharamia unaondelea Dubai ukiwa na mada ya "tishio la kimataifa, kukabiliwa kikanda",mkutano unaojaribu kupata mtazamo wa pamoja wa kimataifa kukabili tatizo la uharamia.

Ban amesema kazi ya kundi la kimataifa linalopambana na uharamia ni muhimu, kuwezesha majadiliano na kuratibu mapambano miongoni mwa mataifa, mashirika, serikali ya mpito, wadau wa kikanda na melizinazoshika doria.