Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yaanzisha mpango kudhibiti homa ya mafua

WHO yaanzisha mpango kudhibiti homa ya mafua

Mapendekezo yaliyofikiwa mwishoni mwa juma ambayo pia yanaungwa mkono na Umoja wa Mataifa yanatazamia kutoa mchango mkubwa wa kudhibiti kuenea kwa ugonjwa wa mafua ya nguruwe iwapo virusi vya ugonjwa huo vitaibuka tena.

Mpango huo unaoratibiwa na shirika la afya ulimwenguni WHO imeweka vipaumbele vyenye nguvu ya kisheria na pia kuwekwa kwa maabara ambazo zinahifadhi vinakilishi vya virusi hivyo umekusudia kutoa elimu ya ufahamu ambayo itasaidia pakubwa iwapo virusi hivyo vitajitokeza.

 

Taarifa ya WHO imesema kuwa kwa kuanisha wajibu na nafasi ya kila mhusika kwenye mpango huo, dunia inasalia kwenye matarajio chanja ya kukabiliana na kuenea kwa virusi hivyo.

 

Makubalino hayo yamefikiwa mwishoni mwa juma wakati wataalamu kutoka WHO na nchi wanachama walipokutana kwa pamoja na kujadiliana kwa kina haja ya kuweka dira ya pamoja ambayo itaweka shabaya ya kukabiliana na mlipuko wa virusi hivyo.