Skip to main content

UM wakaribisha wito wa mkutano wa maridhiano Somalia

UM wakaribisha wito wa mkutano wa maridhiano Somalia

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga amekaribisha wito wa serikali ya mpito ya Somalia wa kufanyika mkutano wa maridhiano ndani ya Somalia mwezi Juni mwaka huu.

Mahiga amesema atahudhuria mkutano huo na kuishawishi jumuiya ya kimataifa kufanya vivyo hivyo. Mahiga amekutana pia na Rais wa Somalia Sheikh Sharif Sheikh Ahmed nchini Tanzania ambako Rais Sharif Ahmed alikwenda kukutana na Rais Jakaya Kikwete.

Balozi Mahiga amemfahamisha Rais Sharif kuhusu mkutano uliokamilizika mjini Nairobi naye Rais Sharif ameiambia jumuiya ya Wasomali kwamba yuko tayari kuhusisha kundi la Al-Shabaab kwenye mazungumzo ya amani endapo kundi hilo litakuwa tayari kuachana na machafuko.