Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kuongeza uwepo wa misaada ya kibinadamu nchini Libya

UM kuongeza uwepo wa misaada ya kibinadamu nchini Libya

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA linasema mapigano makali yanaendelea Misrata Libya, na kusababisha idadi ya vifo isiyojulikana na uharibifu mkubwa wa miundombinu.

Mratibu wa OCHA Valerie Amos na mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu nchini Libya Abdul llah Al-Khatib jana walizuru mji wa Tripol na kukutana na maafisa wa serikali akiwemo waziri mkuu Dr Mahmoud Al-Baghdadi na waziri wa mambo ya nje Abdel Ati Al-Obeid.

Maafisa hao wa Umoja wa Mataifa wamerejea kulaani vikali matumizi ya nguvu dhidi ya raia , kuacha mara moja mashambulizi ya kijeshi na kuruhusu msaada wa kibinadamu kwa wanaouhitaji.

Pia wameitaka serikali kutekeleza azimio la baraza la usalama namba 1970 na 1973 kwa kusitisha mapigano mara moja na kuanza mchakato wa kisiasa kwa kuzingatia matakwa ya wananchi.