Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yawanusuru wahamiaji 1000 Misrata Libya

IOM yawanusuru wahamiaji 1000 Misrata Libya

Mashirika ya kibinadamu ikiwa ni pamoja na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM yamekuwa yakitoa msaada na kuwahamisha maelfu ya wahamiaji waliojikuta wamekwama mjini humo kutokana na mapigano.

Zaidi ya wahamiaji 1200 wamehamishwa mwishoni mwa wiki na leo IOM imewahamisha wahamiaji 1000, wakiwemo raia 650 wa Ghana, 100 wa Libya na wengine kutoka Ufilipino na Ukraine.

Miongoni mwa wahamiaji hao ni wanawake na watoto na 23 majeruhi kama anavyofafanua Jumbe Omari Jumbe afisa wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)