Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wagomea wa uongozi FAO wafafanua ajenda zao

Wagomea wa uongozi FAO wafafanua ajenda zao

Wagombea wa nafasi ya uongozi wa shirika la umoja wa mataifa linalohusika na chakula na kilimo FAO leo wanatazamiwa kuelezea vipaumbele vyao wakati watakapojieleza mbele ya kusanyiko maalumu mjini Rome.

Wagombea hao sita ambao wamepitishwa kuwania nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, wanatazamiwa kuelezea mipango hiyo itayoakisi kama watafanikiwa kushika wadhifa huo watalifanyia nini shirika hilo.

Zoezi la uchaguzi linatazamiwa kufanyika kwenye mkutano wa mwaka wa FAO ambao utafanyika kuanzia June 25 hadi July 2 mjini Rome ukihudhuriwa na 191.

Nafasi hiyo inayowaniwa inashikiliwa na Jacques Diouf ambaye anatazamiwa kustaafu mwishoni mwa mwaka huu 2011 baada ya kumaliza muhula wake.