Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanamuziki wa Mali wawa mabalozi wa WFP dhidi ya njaa

Wanamuziki wa Mali wawa mabalozi wa WFP dhidi ya njaa

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP leo limewatangaza wanamuziki mashuhuri kutoka nchini Mali kuwa mabalozi wema dhidi ya njaa.

Wanamuziki hao wawili wajulikanao kama Amadou Bagayako na Maria Doumbia watakuwa na jukumu la kuelimisha watu wa Ulaya kuhusu tatizo la kimataifa la njaa na juhudi za WFP na muungano wa Ulaya kupambana nalo.

Wanamuziki hao waliowahi kushinda tuzo wote ni watu wasioona na ni mke na mume, pia ni mabalozi wa kwanza wa WFP kuteuliwa kuelimisha kuhusu njaa kwa niaba ya WFP na tume ya msaada wa kibinadamu na idara ya ulinzi ya muungano wa Ulaya ECHO.

Wanamuziki hao wamerea kutoka Haiti ambako wamezuru miradi mbalimbali ya WFP inayofadhiliwa na muungano wa Ulaya. Wakiwa Haiti wamekutana na kina mama wajawazito na wanaonyonyesha ambapo kina mama 25,000 wanapata msaada wa lishe kutoka kwa WFP tangu tetemeko la Januari 2010.