Ari ya Waivory Coast ndio inaamua hatma yao:Choi

Ari ya Waivory Coast ndio inaamua hatma yao:Choi

Ivory Coast inadhihirisha mafanikio ya kiu ya watu kuamua kupigania hatma yao kwa msaada wa kimataifa amesema mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo UNOCI, bwana Y.J Choi.

Akitoa taarifa kwenye baraza la Umoja wa Mataifa kwa njia ya video kutoka mjini Abdjan wakati baraza hilo lilipojadili hali ya Ivory Coast bwana Choi amesema haikuwa lazima kuzuka kwa machafuko baada ya uchaguzi mkuu nchini humo na kudumu kwa zaidi ya miezi mine.

Amesema mamilioni ya watu wamelazimika kuzikimbia nyumba zao, wengi wamepoteza maisha na mfumo mzima wa maisha umebadilika. Lakini ameongeza kufuatia kujisalimisha kwa Bwana Laurent Gbagbo siku ya Jumatatu wiki hii ukurasa umefungwa katika historia ya nchi hiyo na mwingine umefunguliwa.

(SAUTI YA Y.J.CHOI)