Skip to main content

Kuna haja ya kujumisha Wasomali wote kutafuta amani:Mahiga

Kuna haja ya kujumisha Wasomali wote kutafuta amani:Mahiga

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga amesema mkutano wa ngazi ya juu uliomalika jioni hii mjini Nairobi kwa kujadili suala la Somalia umemalizika kwa mafanikio.

Mkutano huo uliwaleta pamoja wadau mbalimbali ikiwemo serikali ya mpito ya Somalia iliyoongozwa na spika wa bunge, Rais Farole na Alin kutoka Puntland na Galmudug, na wawakilishi wa jamii mbalimbali za Kisomali.

Pia washiriki wa jumuiya ya kimataifa, Muungano wa Afrika, Muungano wa Ulaya, mwenyekiti wa IGAD, jumuiya ya nchi za Kiarabu na OIC.  Mada mbalimbali zimejadiliwa na kubadilishana mawazo, na kisha kutoka na makubaliano kadhaa ikiwemo haja ya kumaliza serikali ya mpito kwa mujibu wa mkataba na kuitisha uchaguzi wa Rais na spika wa bunge mwezi Agosti mwaka huu.

Pia imependekezwa kuongeza muda wa bunge la mpito kwa miaka miwili kama kigezo cha kukamilisha majukumu yaliyosalia na kuandaa uchaguzi wa kitaifa. Kuimarisha usalama na juhudi za kukabiliana na itikadi kali, kuongez kasi ya mchakato wa katiba mpya na kuongeza msaada haraka kwa maeneo yaliyoghubikwa na machafuko kama Moghadishu.

Zaidi ya yote wameafikiana kuwaWasomali wote wanastahili kuhusishwa katika mchakato mzima wa suluhisho la amani ya kudumu nchini mwao. Balozi Mahiga amesema huu ni mwanzo na kutakuwa na mikutano mingine ya kufuatilia makubaliano waliyofikia.