Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNEP yapongeza hatua za uchumi unaojali mazingira

UNEP yapongeza hatua za uchumi unaojali mazingira

Zaidi ya wajumbe 200 wamekutana kwa ajili ya kujadilia njia bora itayozisaidia nchi za Afrika kufanikisha mpango wa maendeleo ya uchumi unaojali mazingira.

Mkutano huo ambao umeandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mazingira UNEP pamoja na washindi wa tuzo la SEED umejadiliwa kwa kina hatua zinazopigwa na nchi za Afrika kufikia shabaya ya kuendesha mipango ya uchumi unajali mazingira.

 

Mada nyingine iliyopewa uzito kwenye mkutano huo uliofanyika Pretoria Afrika Kusini, ni kwa kiwango gani nchi za Afrika zinaweza kutengeneza sera ambazo zitasukuma mbele muundo wa uchumi unaojali mazingira.

 

Hata hivyo UNEP imepongeza hatua za ubunifu zinazoendelea kuchukuliwa na wajasiliamali ambao walijitokeza kwa wingi kushiriki shindano la mazingira na baadaye kuibuka washindi.