Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makao makuu ya UM yanafanyiwa ukarabati

Makao makuu ya UM yanafanyiwa ukarabati

Umoja wa Mataifa unakusudia kufanyia ukarabati makao makuu yake mjini New York hatua ambayo itahusisha pia umarishaji wa mifumo ya kiusalama.

Mratibu wa mpango huo Michael Adlerstein amesema kuwa ukarabati huo unatazamiwa  kubadilisha muonekano na pahala ambako jengo la Umoja huo lilipo.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari wakati akiwapa taarifa za maendeleo juu  ya mradi huo, Michael amesema kuwa kuna umuhimu wa kufanyia marekebisho mfumo  mzima wa jengo hilo ili kwenda sambamba na mazingira ya wakati huo.

Suala la uimarishwaji wa mifumo ya usalama ni eneo jingine ambalo limepewa kipaumbele cha pekee kwenye ukarabati huo.