Wakati ripoti ya UM ikielezea mafanikio na mapungufu Ban atoa wito wa hatua madhubuti kupambana na ukimwi

31 Machi 2011

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kwa ushirikiano na mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Ukimwi UNAIDS Michel Sidibe leo wamezindua rasmi ripoti ya Ukimwi mjini Nairobi Kenya.

Ripoti hiyo inaonyesha kwamba uwekezaji katika vita dhidi ya ukimwi unaanza kuzaa matunda. Inaonyesha maambukizi mapya duniani yanapungua, fursa ya kupata dawa inaongezeka na kumekuwa na hatua kubwa katika kupunguza maambukizi ya HIV kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Mwandishi wetu Jason Nyakundi alikuwepo kwenye uzindizo huo na kuandaa ripoti ifuatayo.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amesema kuwa unyanyapaa, ubaguzi na kutokuwepo kwa usawa wa kijinsia ni kati ya vizingiti vinavyotatiza juhudi za kupambana na ugonjwa wa ukimwi duniani. Akiongea alipokuwa akitoa ripoti kuhusu ugonjwa wa ukimwi mjini Nairobi nchini Kenya Ban amesema kuwa ifikapo mwaka 2015 maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi kupitia kwa ngono yanastahili kupunguzwa kwa nusu, kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto , kupunguza kwa nusu vifo vinavyosababishwa na ugonjwa wa ukimwi, kuwapa matibabu takriban watu milioni 13 na pia kutoa marufuku ya wanaougua ugonjwa wa ukimwi kusafiri kwenda nchini zingine.

Hata hivyo Ban amesema kuwa kumekuwa na tofauti kubwa kati ya sasa na wakati ugonjwa huo ulipogunduliwa miaka 30 iliyopita

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Ban ameongeza kuwa ikiwa jitahada za sasa za kukabiliana na ugonjwa wa ukimwi zitaendelea basi kutakuwa na ulimwengu usio na maambukizi mapya ya ugpnjwa wa ukimwi , ubaguzi na pia vifo vinavyosababishwa na ugonjwa huu.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter