Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mcheza filamu Liam Neeson awa balozi mwema wa UNICEF

Mcheza filamu Liam Neeson awa balozi mwema wa UNICEF

Mcheza filamu Liam Neeson hii leo ametangazwa kama balozi mwema wa shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF

Hatua hiyo imekuja kutokana na jitihada zake za kuwasaidia na kubadili maisha ya watoto kote duniani wanaokabiliwa na umaskini, magonjwa, dhuluma pamoja na waliotengwa. Mshindi huyo wa tuzo la Oscar amekuwa akiunga mkono UNICEF tangu mwaka 1997 kama moja ya wajibu wake kama balozi wake nchini Ireland.

Mkurugenzi mkuu wa UNICEF Antony Lake amesema kuwa Liam Neeson sio tu mcheza filamu wa kutumbuiza bali pia hujumuisha masuala ya kibinadamu.