Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukweli ni muhimu kwa waathirika wa ukiukwaji haki:Ban

Ukweli ni muhimu kwa waathirika wa ukiukwaji haki:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ameelezea haki ya waathirika wa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na familia zao kujua ukweli wa kilichotokea.

Katika ujumbe maalumu wa siku ya kimataifa ya haki ya kujua ukweli kwa wahanga wa ukiukwaji wa haki za binadamu, Ban amesema wahanga hao wana haki ya kujua mazingira yaliyosababishiwa haki zao kukiukwa, kwa nini walifanyiwa hivyo na ni watu gani waliohusika kukiuka haki zao za binadamu. George Njogopa na ripoti kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Katibu Mkuu Ban amesema haki ya kufikiwa na ukweli kwa hivi sasa ni suala lisilokwepeka tena na tayari limepata baraka zote toka jumuiya za kimataifa ikiwemo kuasisiwa kwa mkataba wa kimataifa juu ya haki za kulindwa kwa binadamu kutumbukia kwenye majanga ambayo imeanza kufanya kazi tangu disemba mwaka jana 2010.

Lakini pia imesisitizwa kuwa kuwepo kwa hali ya ukweli na uwazi, ni suluhisho mujarabu la kukabiliana na matukio ya uvunjifu wa kupindukia haki za binadamu kwani wahusika wake ni rahisi kuwajibika.