Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uungaji mkono wa nchi za Kiarabu ni muhimu kutekeleza azimio la baraza la usalama Libya:Ban

Uungaji mkono wa nchi za Kiarabu ni muhimu kutekeleza azimio la baraza la usalama Libya:Ban

Ushirikiano baina ya Umoja wa Mataifa na jumuiya ya nchi za Kiarabu ni muhimu sana kama kweli demokrasia itachukua mkono katika ukanda wa nchi za Kiarabu.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika mkutano wake na Katibu Mkuu wa jumuiya ya nchi za Kiarabu Amr Moussa mjini Cairo Misri.

Katika mkutano wao ambao umejadili kwa kina hali nzima inayoendelea Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati hasa Libya, Bahrain na Yemen Ban amesema Umoja wa Mataifa utaendelea kuchukua hatua za haraka kumaliza mapigano na kutoa msaada wa kibinadamu unaohitajika.

Ameongeza kuwa ni muhimu kutumia njia za amani kuhakikisha umoja wa kitaifa, utulivu na kuweka mazingira bora ya kuleta mabadiliko.