Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF inaomba dola milioni 51 kusaidia wanawake na watoto

UNICEF inaomba dola milioni 51 kusaidia wanawake na watoto

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linaomba dola milioni 51 ili kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya wanawake na watoto walioathirika na machafuko ya baada ya uchaguzi nchini Ivory Coast na Liberia.

Zaidi ya Waivory Coast 300,000 wamefanywa kuwa wakimbizi wa ndani na machafuko hayo ambapo asilimia 60 ni wanawake na watoto ambapo kila mara machafuko yanapozuka hujikuta ndio waathirika wakubwa. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Hali inavyoonekana mvutano huu wa madarani hauwezi kupata tiba kwa wakati huu , na hivyo kuongeza hali ya wasiwasi kwa wakazi zaidi ya milioni moja ambao wapo mashakani kukosa huduma ya maji safi na salama.

Kuna wasiwasi pia kuvurugika kwa huduma za kiafya kunakosababishwa na upungufu wa wafanyakazi pamoja na vifaa vya kitabibu. Hali jumla ya mambo siyo ya kuridhisha na inaarifiwa kwamba zaidi ya watoto 800,000 wamesimama kwenda shule kufuatiwa kufungwa kwa shule hizo. Idadi ya wakimbizi wanaokimbilia nchi jirani ya Liberia imeongezeka na sasa wamefikia 90,000.