Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza kuepusha vikwazo dhidi ya shughuli za kibinadamu Somalia

Baraza kuepusha vikwazo dhidi ya shughuli za kibinadamu Somalia

Baraza la uslama la Umoja wa Mataifa limepiga kura kusamehe vikwazo dhidi ya mashirika yanayofanya operesheni za kibinadamu nchini Somalia.

Hii ni kutokana na azimio linaloyataka mataifa kuweka vikwazo vya fedha katika makundi au watu binafsi ambao wanaingilia juhudi za kuleta amani na utulivu katika nchi hiyo ya pembe ya Afrika.

Chini ya azimio hilo la 2008, nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wana wajibu wa kuzuia fedha, samani au rasilimali za kiuchumi ambazo ziko katika nchi zao zinazomilikiwa na watu au kundi linaloendesha shughuli za kutishia amani, utulivu au operesheni za kibinadamu nchini Somalia. Jason Nyakundi ana taarifa kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)