Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji zaidi ya 50,000 wahamishwa Libya na IOM/UNHCR

Wahamiaji zaidi ya 50,000 wahamishwa Libya na IOM/UNHCR

Operesheni ya pamoja ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM imesaidia kuwahamisha maelfu ya wahamiaji kutoka nchini Libya.

Operesheni hiyo inayofanyika kwa msaada wa nchi mbalimbali imefanikiwa kuwahamisha wahamiaji zaidi ya 50,000 waliokuwa wamekwama kwenye makambi ya mpakani mwa Tunisia na Libya. Maelfu kwa maelfu wengine wamerejeshwa makwao kwa kutumia ndege na meli zilizotolewa na serikali zao.

Mkurugenzi mkuu wa IOM William Lacy Swing amesema operesheni hiyo ni moja ya operesheni kubwa kabisa katika historia ya kuwahamisha wakimbizi na wahamiaji. Melissa Fleming ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA MELISSA FLEMING)