Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya mapigano raia wa Mauritania waendelea kuhamishwa Ivory Coast

Licha ya mapigano raia wa Mauritania waendelea kuhamishwa Ivory Coast

Zoezi la kuwakwamua raia wa Mauritanian walioko nchini Ivory Coast litaendelea kutekelezwa licha kuzuka upya machafuko katika mjii mkuu wa Abidjan.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM tayari limeanza kuwaondosha raia hao wanaofikia 1,000 kwa kutumia usafiri wa basi. Hata hivyo vitendo vya ghasia vilivyoripotiwa kujiri katika ofisi za ubalozi wa Mauritania nchini humo vimekwaza kwa muda juhudi za kuwanusuru raia hao ambao wamechukua hifadhi kwenye eneo hilo.

Hali ya machafuko iliyozuka wiki chache zilizopita, imesababisha mamia ya watu kukimbia makazi yao na wengine wamekwama kwenye maeneo ya mji wa Abidjan.