Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu zaidi ya 250,000 wamekimbia Libya:IOM

Watu zaidi ya 250,000 wamekimbia Libya:IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limesema zaidi ya watu 250,000 wakiwemo wahamiaji wa kigeni 21,000 wamekimbia nchini Libya tangu kuanza kwa machafuko ya kutaka kuuondoa utawala wa Qadhafi madarakani mwezi Februari.

Hata hivyo IOM inasema shughuli za usafirishaji wa wahamiaji hao zitakumbwa na dosari kkatika siku zijazo kutokana na upungufu wa fedha. George Njogopa na taarifa kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Ripoti zinaonyesha kwamba kwa siku zaidi ya watu 6,000 wanaondoka nchini humo na kuingia katika nchi za Tunisia na Misri na kunawasiwasi kwamba huenda idadi hiyo ikaongezeka katika siku za usoni. Shirika la umoja wa mataifa linalohusika na uhamiaji IOM linakadiria kwamba huenda likazidiwa na kukosa rasilimali kwa ajili ya kuwagharimia watu hao ambao ni raia wa Bangladesh wenye kiu ya kureja makwao,

 

Kulingana na Mkurugenzi wa kikosi kazi wa shirika hilo Mohammed Abdiker, huenda huduma za kuwasuru watu hao zikafungwa kwa muda kutokana na kukosa fedha za kutosha kuwasafirisha wahamiaji hao. IOM inahitaji kiasi cha dola za kimarekani milioni 49.9 ili kusukuma mbele juhudi za kuwakwamua zaidi ya wahamiaji 65,000 waliokwama huko Libya.