Skip to main content

UM umetuma salamu za rambirambi na kuahidi msaada baada ya tetemeko na tsunami kuikumba Japan

UM umetuma salamu za rambirambi na kuahidi msaada baada ya tetemeko na tsunami kuikumba Japan

Tetemeko la ukubwa wa vipimo vya rishita 8.9 limeikumba Japan na kusababisha tsunami iliyoathiri ukanda mzima wa Pacific.

Mamia ya watu wamearifiwa kufariki dunia na idadi inatarajiwa kuongezeka. Tetemeko hilo lililoelezwa kuwa kubwa kabisa kuwahi kuikumba Japan tangu kuanza kuwekwa kumbukumbu za matetemeko , limesababisha uharibifu mkubwa kwenye kitovu cha tetemeko hilo ambako ni kilometa 250 Kaskazini Mashariki mwa Tokyo.

Maafisa wa serikali ya Japan wametangaza hali ya tahadhari kwenye mitambo yake ya nyuklia hasa Fukushima Daiichi ambayo sasa imefungwa, lakini hakuna taarifa zozote za kusambaa kwa mionzi. Akizungumzia tetemeko hilo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema Umoja wa Mataifa unafuatilia kwa karibu hali hiyo hasa kwa kuwa matetemeko mengine madogomadogo yanashuhudiwa kwenye ukanda wa Pacific.

Amesema dunia imeshtushwa na hali hiyo na Umoja wa Mataifa uko tayari kuisaidia Japan kwa kila hali.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)