Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu ya wahamiaji wamerejeshwa makwao ingawa kuna Wasomali wanaosubiri kwa kupelekwa:IOM

Maelfu ya wahamiaji wamerejeshwa makwao ingawa kuna Wasomali wanaosubiri kwa kupelekwa:IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linasema idadi ya wahamiaji wanaovuka mpaka kutoka Libya na kuingia Tunisia imepungua na wanahisi ni kutokana na mapigano yanayoendelea nchini Libya.

Hata hivyo shirika hilo linasema bado linahitaji msaada wa fedha kuweza kukidhi mahitaji ya maelfu ya wahamiaji ambao wengine wanasubiri kurejea makao na wengine kutafutiwa kwa kwenda. Kwa mujibu wa shirika hilo hadi sasa maelfu ya wahamiaji waliokuwa wakifanya kazi nchini humo kutoka Misri wamerejeshwa makwao, na wengine kutoka Bangladesh, India, Pakistan na Afrika wanaendelea kusafirishwa.

Hata hivyo kuna baadhi ya wahamiaji ambao baada ya kukimbia Libya hawajui wapi watakapopelekwa kutokana na kwamba nchi zao zinakabiliwa na machafuko. Flora Nducha amezungumza na afisa habari na mawasiliano wa IOM Jumbe Omar Jumbe na mmoja wa wahamiaji wa  Somalia ambaye ni  ni Mohamed Abdallah miongoni mwa Wasomali 300 walioko kwenye mpaka wa Al Jadir ras Jadil.

(MAHOJIANO NA JUMBE NA ABDULLAH)