Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM leo imesafirisha idadi kuwa na wahamiaji wa Kiafrika kutoka Libya

IOM leo imesafirisha idadi kuwa na wahamiaji wa Kiafrika kutoka Libya

Maelfu ya wahamiaji wa Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara leo wamekuwa wakirejeshwa nyumbani kutoka Libya.

Shirika la Kimataifa la wahamiaji IOM linasema wahamiaji wengi wamefanikiwa kutoroka Libya wanakohofia usalama wao na kufika maeneo ya mipakani kupata msaada wa IOM. Wengi wa wahamiaji hao wanatoka Nigeria, Ghana, Mali, Sudan, Guinea, Niger, Senegal, Somalia na Cameroon.

Kwa mujibu wa afisa habari na wasiliano wa IOm Jumbe Omari Jumbe zoezi la kuwasafirisha limeshika kasi na linakwenda haraka. akizungumza na Alice Kariuki wa Idhaa hii amesema hali inabadilika haraka kwenye mpaka wa tunisia na Libya wanakosafirisha wahamiaji hao.

(MAHOJIANO NA JUMBE OMARI JUMBE)