Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM una mchango mkubwa sio kwa misaada tuu bali pia kuelimisha jamii

UM una mchango mkubwa sio kwa misaada tuu bali pia kuelimisha jamii

Umoja wa Mataifa na mashirika yake mbalimbali umekuwa ukiendelea kutoa mchango mkubwa duniani katika njanja nyingi zikiwemo za kiuchumi, kijamii, kisiasa na kitamaduni.

Mbali ya kutoa msaada na huduma palinapotokea matatizo, pia kupitia taasisi mbalimbali ikiwemo Radio ya Umoja wa Mataifa umekuwa ukielimisha jamii, kuwapasha habari na kuwashirikisha kwa njia moja au nyingine. Hivi karibuni vijana kutoka chuo kikuu cha kimataifa cha Kimarekani kilichopo mjini Nairobi Kenya (USIU) walikuja Marekani kwa mwaliko rasmi wa chuo kikuu cha Harvard kilichopo Massachusetts. Walifika kutembelea Umoja wa Mataifa na kuzungumza na Alice Kariuki wa Redio ya UM.

Wanazuoni hao Raymond Maro, Josephine Njambi, Sia Ernest Maliya na mwalimu wao Moses Onyango pia walizuru Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa na kuzungumza  na Alice Kariuki kuhusu mchango wa Radio ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Mataifa kwa ujumla.

(MAHOJIANO NA ALICE KARIUKI)