Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vitendo vya ubakaji Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo vimefurutu ada

Vitendo vya ubakaji Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo vimefurutu ada

Wanawake kwa maelfu hubakwa kila uchao na sasa sio mashariki mwa nchi hiyo tuu ambako makundi ya wanamgambo wenye silaha wanakabiliana na serikali ya Rais Joseph Kabila, bali nchi nzima.

UNHCR inasema inajitahidi kuwasaidia waathirika lakini hali inatia hofu. Serikali kwa upande wake haijabwaga manyanga lakini inaelekea mzigo ni mzito na hakuna dalili la tatizo hilo kuisha leo wala kesho.

Labda unajiuliza  nini kiini cha tatizo hili? kwa nini haliishi licha ya juhudi zilizopo? na ni kubwa kiasi gani? Bi eva Bazaiba seneta na mwanaharakati wa haki za wanawake anatueleza. Na unaweza kusikiliza mahojiano haya katika tovuti hii www.unmultmedia.org