Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ateuwa mwakilishi kwa matatizo ya Libya

Ban ateuwa mwakilishi kwa matatizo ya Libya

Mwanadiplomasia wa zamani wa ngazi za juu wa Jordan ameteuliwa kuwa mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon Libya ili kukabiliana na matatizo yanayolikumba taifa hilo la Afrika ya Kasakazini kwa sasa.

Waziri huyo wa zamani wa mambo ya nje wa Jordan Abdelilah Al-Khatib atakuja New York katika siku chache zijazo kabla ya kuanza majukumu yake Libya. Bwana Khatib atakutana na serikali ya Libya mjini Tripol kuhusu hali ya kibinadamu pamoja na matatizo mengine .

Aliteuliwa jana Jumapili na Ban Ki-moon siku ambayo Ban alizungumza kwa njia ya simu na waziri wa mambo ya nje wa Libya Musa Kusa na kumwambia Tripoli lazima itemize wajibu wake wa kuwalinda raia wake. Ban amesisitiza kwa wale wanaokiuka haki za kimataifa za kibinadamu na sheria au kutekeleza uhalifu ni lazima wawajibishwe.