Wahisani wakutana Geneva kuomba fedha kuisaidia Libya

1 Machi 2011

Mashirika ya kimataifa ya misaada yanaongeza juhudi kuwasadia maelfu ya wafanyakazi wahamiaji waliokwama kwenye mpaka wa baina ya Libya, Misri na Tunisia.

Mashirika hayo yanakutana mjini Geneva ili kuomba fedha za kuwasaidia wahamiaji hao ambao wanakimbia machafuko nchini Libya. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema hali kwenye mpaka wa Tunisia ni mbaya sana .

Zaidi ya watu 14,000 ambao ni wahamiaji wamearifiwa kuvuka mpaka jana Jumatatu na idadi kama hiyo au zaidi inatarahjiwa leo. Melisa Fleming ni msemaji wa UNHCR

(SAUTI YA MELISA FLEMING)

UNHCR inaweka mahema 1000 ili kutoa malazi ya dharura kwa watu takribani 12,000 kwenye mpaka wa Libya. Mkutano wa leo wa wahisani unashirikisha mashirika ya OCHA, UNHCR, na IOM.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter