Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNICEF azuru DRC kutathimini hali ya watoto

Mkuu wa UNICEF azuru DRC kutathimini hali ya watoto

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Athony Lake amewasili mjini Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hii leo ili kukutana na maafisa wa serikali na kuzuru maeneo ambayo maafisa wa afya wanakabiliana na mlipuko unaosambaa haraka wa polio.

Katika ziara hiyo ya siku nne bwana Lake atatathimini hatua iliyopigwa katika kuokoa maisha ya watoto na kuwalinda na pia kuangalia athari zinazoendelea kusababishwa na matatizo ya ukosefu wa usalama nchini humo.

DR Congo imeshuhudia mlipuko mpya wa polio uliotia dosari juhudi za kimataifa za kutokomeza maradhi hayo. Tangu Januri mwaka jana hadi Januari mwaka huu visa vipya 112 vya polio vimeripotiwa.