Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali yazidi kuwa mbaya kwenye mpaka wa Tunisia na Libya

Hali yazidi kuwa mbaya kwenye mpaka wa Tunisia na Libya

Hali imeelezewa kuzidi kuwa mbaya kwenye mpaka baina ya Libya na Tunisia huku idadi ya watu ikiongezeka.

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP ambalo linagawa chakula cha msaada linasema watu wanaovuka mpaka kila siku inaongezeka na huduma ni ndogo .  Mkurugenzi wa WFP Josette Sheeran anazuru eneo hilo la mpakani na atkutana na maafisa wa serikali kujadili mahitaji ya kibinadamu kwa wanaokimbia machafuko na athari zake hasa kwa wanawake na watoto.

Nalo shirika la afya duniani WHO linasema idadi ya wanaokufa na kujeruhiwa inapanda kila siku na imeweka zahanati za dharura 20, magari ya wagonjwa 26 kwa ajili ya kuhudumia majeruhi. Fadela Chaib ni msemaji wa WHO.

(SAUTI YA FADELA CHAIB)