Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Washinda tuzo la Sasakawa

Washinda tuzo la Sasakawa

Miradi miwili iliyokuwa na shabaya ya kuhifadhi mazingira na kukaribisha maendeleo endelevu katika maeneo ya vijijini huko Latin Amerika na Asia imefaulu kushinda tuzo la UNEP ijulikanayo Sasakawa.

The Asociación Forestal Integral San Andrés, Petén (AFISAP)ya Guatemala na Manahari  Development Institute ya Nepal, ndiyo walioibuka washindi wa tuzo hiyo iliyoandaliwa na shirika la umoja wa mataifa linalohusika na mazingira UNEP.

 

Dhima kubwa ya shindano hilo ni kuzihamasisha taasisi pamoja na mashirika mengine kuendesha miradi ambayo itahakikisha inatilia uzito mapinduzi ya uchumi wa kijani kama njia muafaka ya ukuzaji uchumi.

 

Takwimu zilizopo zinaonyesha kwamba ulimwengu unakabiliwa na kitisho cha kupoteza kiasi cha dola za kimarekani trilioni 2.5 hadi 4.5 kila mwaka kutokana na athari za kupotea kwa misitu