Norway na Ujerumani zahaidi kutoa fungu la fedha kusaidia FAO kukabili tatizo la mabadiliko ya tabia nchi

15 Februari 2011

Ujerumani na Norway zimehaidi kutoa kiasi cha dola za kimarekani milioni 5 kusaidia mpango unaoendeshwa na shirika la umoja wa mataifa la chakula na kilimo FAO ambao inakusudia kusambaza taarifa duniani kote kuhusiana na mradi wa mapinduzi ya kijani ili kulinda mazingira

Mpango huo ni sehemu ya Umoja wa Mataifa wa kupunguza kiwango cha gesi kinachozalishwa angani ambayo inaharibu mazingira na kukaribisha tatizo la mabadiliko ya tabia nchi.

 

FAO imedhamiria kusambaza taarifa za mradi huo wa nyumba za kijani kwenye mitandao mbalimbali ili iwe rahisi kufikiwa na walengwa na kuianisha njia nyingine mujaribu zinazofaa kuhusiana na mapinduzi ya kijani.

 

Hatua hiyo inatazamiwa kuzifaa serikali, wahisani wa maendeleo pamoja na wakulima ambao watatumia fursa hiyo kukusanya taarifa zitakazowawezesha kubuni miradi kabla ya kupewa ufadhili wa fedha.

 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter