Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR imeaanza kuwasaidia wakimbizi walioko Misri

UNHCR imeaanza kuwasaidia wakimbizi walioko Misri

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeanza kutoa misaada ya kifedha na ya kimatibabu kwa wakimbizi mjini Cairo nchini Misri ambao wanaishi katika hali mbaya wakati huu.

Pia UNHCR imebuni njia ya mawasialiano kwa njia ya simu ambapo wakimbizi wanaweza kupata usaidizi. Kwa sasa kuna wakimbizji pamoja na watafuta hifadhi 107,000 nchini Misri ambapo 39,680 kati yao wamesajiliwa na UNHCR .

Wengi wa wakimbizi hao wanatoka nchini Sudan, Iraq, Somalia, Ethiopia na Eritrea.  Adrian Edward ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)