Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yawasaidia Wasudan Kusini wanaorejea nyumbani

UNHCR yawasaidia Wasudan Kusini wanaorejea nyumbani

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa idadi ya wenyeji wa Sudan Kusini wanaorejea nyumbani inatarajiwa kuongezeka kwa zaidi ya watu 800,000 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Tangu Disemba mwaka uliopita wenyeji 200,000 wa Sudan Kusini wamerejea nyumbani kutoka kaskazini kutokana na hamu ya kutaka kuishi kwenye taifa jipya la Sudan Kusini. UNHCR inasema kuwa wenyeji wa Sudan kusini walihofia uraia wao iwapo wangeendelea kuishi katika eneo la Sudan Kaskazini .

Adrian Edwards kutoka UNHCR anasema kuwa wanaorejea nyumbani wanaongezea changomoto za kibinadamu zinazowakabili wenyeji wa Sudan kusini. UNHCR imeoa wito wa msaada wa dola milioni 53.4 kuwasaidia watu hao.

(SAUTI YA ANDREJ MAHECIC)