Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP imenunua chakula kingi katika nchi zinazoendelea

WFP imenunua chakula kingi katika nchi zinazoendelea

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linasema lilipokea bidhaa ya chakula za gharama ya dola bilioni 1.25 mwaka uliopita na kununua chakula kingi zaidi kuwahi kununuliwa kutoka kwenye nchi zinazoendelea.

Chakula hicho kilitoka kwenye mataifa 96 yakiwemo Ethiopia, Vietnam, na Guatemala na kusaidia watu walioathirika na mafuriko nchini Pakistan , walioathirik na tetemeko la ardhi nchini Haiti na ukame katika eneo la Sahel.

Mwaka 2010 WFP ilinunua ngano , mahindi , mchele na pia chakula kingine spesheli ambacho ni muhimu kwa akina na watoto kabla ya kuzaliwa hadi umri wa miaka miwili. Zaidi ya asilimia 80 ya chakula chote kilichonunuliwa na WFP kilitoka kwenye nchi zinazoendelea. Emilia Casella ni kutopka WFP.

(SAUTI YA EMILIA CASELLA)