Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baada ya siku 18 hatimaye Rais Hosni Mubarak ajiuzulu Misri

Baada ya siku 18 hatimaye Rais Hosni Mubarak ajiuzulu Misri

Hatimaye baada ya siku 18 za maandamano ya mamilioni ya watu katika miji mikubwa nchini Misri Rais Hosni Mubaraka amejiuzulu.

Mubarak aliyekuwa madarakani kwa miaka 30 sasa ametangaza kujiuzulu hii leo baada ya kutofanya hivyo Alhamisi siku iliyotarajiwa na wengi kuwa aneondoka. Mubaraka ameagiza baraza la jeshi kushika hatamu kwa sasa na kuandika historia kwa watu takribani milioni 80 wa nchi hiyo.

Kujiuzulu kwake kumetangazwa na makamu wa Rais Omar Suleiman na kuzusha hamasa kubwa kwa mamilioni ya watu waliokuawa wakiangalia tangazo hilo moja kwa moja kupitia televisheni ya taifa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kwa wiki mbili sasa amekuwa akirejea wito wake wa uongozi wa Misri kusikiliza matakwa ya watu kwa njia ya amani na utulivu, kuheshimu haki za binadamu na kuwapa watu uhuru wa kujieleza na kuandamana.