Skip to main content

UM wandaa mazungumzo kuhusu taifa la Macedonia

UM wandaa mazungumzo kuhusu taifa la Macedonia

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa uliotwikwa jukumu la kuongoza mazungumzo kati ya Ugiriki na taifa lililokuwa Yugoslavia ya zamani la Macedonia kwenye mzozo kuhusu jina la taifa hilo umekamilisha mazungumzo ya siku mbili yaliondaliwa mjini New York Marekani na kuhudhuriwa na waakilishi kutoka pande zote mbili.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirky aliwambia waandishi wa habari kuwa sababu ya mkutano huo ni kuwapa fursa waakilishi kutoka pande zote mbili kubadilishana misimamo ya nchi zao kuhusiana na tofauti zilizo kati yao.

Mkutano huo pia ulitaka kubaini iwapo kuna sehemu zilizosalia ambazo zinahitaji kushughulikiwa zaidi ili kuweza kupiga hatua zaidi kwa lengo la kupatikana suluhu kwa haraka kufuatia utata uliopo kuhusu jina.