Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ongezeko la bei ya chakula litakuwa na athari kubwa hatua zisipochukuliwa:Balozi Mchumo

Ongezeko la bei ya chakula litakuwa na athari kubwa hatua zisipochukuliwa:Balozi Mchumo

Wiki hii shirika la Umoja wa mataifa la chakula na kilimo FAO limesema bei ya chakula dunia imefurutu ada mwezi wa Januari mwaka huu

Gharama za chakula kama ngano, mahindi, sukari na mafuta ya kupikia imekuwa ya juu kuliko wakati mwingine wowote. FAO inasema bei zimekuwa zikipanda kwa miezi saba iliyopita na inaonekana itaendelea katika miezi ijayo. Ngano, mahindi, sukari na bidhaa za maziwa imepanda kwa asilimia kati ya 3 na 6 kwa mwezi Januari mwaka huu wa 2011.

Hali hii imesababisha kufanyika kongamano la kimataifa mjini Geneva Uswis kuhusu kupanda kwa bei ya chakula, athari zake na njia za kukabiliana na tatizo hilo. Kongamano hilo limeandaliwa na shirika la Umoja wa mataifa la masuala ya bidhaa na biashara UNCTAD na kuhusisha FAO, shirika la mpango wa chakula duniani WFP na wadau wengine.

Miongoni mwa waliohudhuria ni balozi Ali Mchumo ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa mfuko wa pamoja wa masuala ya bidhaa wa UNCTAD. Amezungumza nwa mwandishi wetu wa Geneva Patrick Maigua na kuanza kumueleza nini sababu kubwa ya kupanda kwa bei ya mazao duniani.

(MAHOJIANO NA BALOZI MCHUMO)