Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali ya Misri isikilize sauti za watu:Somavia

Serikali ya Misri isikilize sauti za watu:Somavia

Mkurugenzi mkuu wa shirika la kazi duniani Juan Somavia ametoa taarifa hii leo akiitaka serikali ya Misri na wadau wote wa amani kufungua njia ya ukurasa mpya wa haki katika historia ya nchi hiyo.

Amesema inasikitisha na kutia simanzi kuona maisha ya watu yanapotea kwa kiasi kikubwa namna hiyo.

ILO imekuwa ikizungumzia ukosefu wa ajira bora nchini Misri na mataifa mengine jirani ambayo ni ya kiwango kikubwa duniani. Amesema kushindwa kushughulikia hali hiyo pamoja na masuala mengine ya msingi kumesababisha tafrani inayoendelea.

Somavia amesema hofu ya ILO Misri ni sheria zinazobana ambazo zimeruhusu kuwepo na shirikisho moja tuu la biashara na kuzuia mashirika huru ya wafanyakazi na jumuiya za wafanyakazi. Amesema ni lazima serikali isikilize matakwa ya watu wake ili kudumisha haki na amani.