Ongezeko la bei ya chakula duniani limefurutu ada Januari mwaka huu:FAO
Shirika la Umoja wa mataifa la chakula na kilimo FAO limesema bei ya chakula dunia imefurutu ada mwezi wa Januari mwaka huu.
Gharama za chakula kama ngano, mahindi, sukari na mafuta ya kupikia imekuwa ya juu kuwahi kutokea katika wakati huu ambapo upatikanaji wake pia umeanza kuwa mgumu. FAO inasema bei zimekuwa zikipanda kwa miezi saba iliyopita na inaonekana itaendelea katika miezi ijayo.
Bei ya ngano, mahindi, sukari na bidhaa za maziwa imepanda kwa asilimia kati ya 3 na 6 kwa mwezi Januari mwaka huu wa 2011. Sababu kubwaya kupanda huko imeelezewa kuwa hali ya hewa ambayo imeathiri uzalishaji katika nchi nyingi. George Njogopa na taarifa kamili.
(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)