Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali lazima zisikilize matakwa ya watu:UM

Serikali lazima zisikilize matakwa ya watu:UM

Matukio yanayoendelea kujitokeza katika nchi kadhaa ni matokeo ya kuchanganyikiwa kwa watu ambao sauti zao hazisikilizwi au zinapuunzwa na serikali.

Wataalamu binafsi wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wanasema katika wiki za karibuni mamilioni ya watu wanaume kwa wanawake katika nchi nyingi zikiwemo Belarus, Yemen, Misri na Tunisia wamekuwa wakielezea gadhabu zao.

Ghadhabu hizo zinahusiana na ukosefu wa fursa za ajira , ukiukwaji wa haki zao za msingi kama chakula na nyumba mambo yaliyochangiwa na ongezeko la bei ya changula na bidhaa zingine. Pia kunyimwa haki za kufanya maamuzi, haki za binadamu, kiraia, kitamaduni, kiuchumi na kisiasa. Jason Nyakundi anaripoti.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)