Skip to main content

Maandamano yaghubikwa na ghasia wakati Rais Hosni Mubarak hatogombea tena urais nchini Misri

Maandamano yaghubikwa na ghasia wakati Rais Hosni Mubarak hatogombea tena urais nchini Misri

Akihutubia taifa jana kupitia televishen amesema amesikitishwa na hali inayoendelea nchini humo na anazingatia matakwa ya wengi.

Uchaguzi mkuu wa Rais unaofanyika kila baada ya miaka sita unatarajiwa mwezi Septemba mwaka huu. Jumanne ya wiki hii malaki ya watu walimiminika katika mitaa ya mji mkuu Cairo, Alexandria, Suez na Sulemania wakimtaka Rais huyo kuachia madaraka na sio kubadili baraza la mawaziri, au kuteua makamu wa Rais.

Kutangaza kwake kuwa hatosisi tena uchaguzi bila kuondoka ni hatua itakayowaridhisha maelfu ya waandamanaji? Na nini hasa kilichowachagiza kuingia mitaani? Nimezungumza na Ismail Mfaume mwandishi habari na mtangazazi wa Radio Cairo Misri ambayo ni washirika wetu

(MAHOJIANO)