Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Asia yaongoza kwa kusafirisha nje vifaa vya ICT:UNCTAD

Asia yaongoza kwa kusafirisha nje vifaa vya ICT:UNCTAD

Ripoti mpya iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa UNCTAD ambayo imezingatia hali ya uchumi kwa mwaka 2009 inaonyesha kuwepo kwa ongezeko la biashara ya habari, mawasiliano na teknolojia ICT kwa nchi za Asia.

Takwimu hizo zinaonyesha kuwa katika kipindi cha mwaka 2009, bidhaa za ICT iliongezeka hadi kufikia kiwango cha asilimia 66.3, ikiwa imepanda kiasi ikilinganishwa na mwaka mmoja nyuma wa 2008 ambacho kiwango chake kilifikia asilimia 63.8

Takwimu hizo zinabainisha kuwa, matatizo yaliyotokana na mkwamo wa uchumi ulioikumba dunia, kumefanya upepo kwa biashara ya ICT kubadilika na kuzifunaisha zaidi nchi za asia ambazo zimesafirisha kwa kiwangi kikubwa katika soko la nje. China ndiyo iliyoshika nafasi ya kwanza kuuza kiwango kikubwa zaidi katika soko la nje, ikifuatiwwa na Hong Kong