Wakati idadi ya watu kufikia bilion 7 vijana wawekewe mipango:UNFPA

Wakati idadi ya watu kufikia bilion 7 vijana wawekewe mipango:UNFPA

Wakati ongezeko la watu duniani likikaribia kufikia bilioni 7 mwaka huu, shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na idadi ya watu UNFPA limetaka serikali kuanza kuunda sera ambazo zinajibu changamoto za kukabiliana na tatizo la umaskini, tatizo ambalo linawaandama zaidi vijana.

UNFPA imesema kuwa kuwekeza kwa vijana hasa katika maeneo yanayohusika na afya ya uzazi na kuwepo kwa usawa wa kijinsia, kunaweza kusaidia kwa nchi nyingi kufikia shabaya ya kusukuma mbele shughuli za ukuzaji uchumi na uletaji wa maendeleo.

Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA amesema kuwa moja ya shabaya ya shirika hilo hivi sasa ni kuendelea kufanya kazi na nchi mbalimbali duniani kote ili kuzikabili changamoto zitokanazo na ongezeko la watu duniani na mkazo ukitiliwa kwa vijana ambao ndiyo walioko kwenye mstari mbaya wa kuathiriwa na ongezeko hilo.

Shirika hilo limehaidi kuanza kuweka vipaumbele vyake ikiwemo kuhakikisha kuwa haki za kinanadamu na utu wa mtu unaendelea kuheshimiwa duniani kote.