Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa UM kuzuru Kenya na Somalia

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa UM kuzuru Kenya na Somalia

Mratibu wa masuala ya kibinadamu na huduma za dharura wa Umoja wa Mataifa bi Valerie Amos anatarajiwa kufanya ziara rasmi nchini Kenya na Somalia kati ya tarehe mosi na tatu mwezi Februari mwaka huu ambapo atakadiria hali ya ukame katika nchi hizo mbili.

Nchini Kenya bi Amos atakutana na waakilishi wa serikali ambapo atatoa shukran zake kwa Kenya kutokana na misaada ya kibinadamu inayochangia na kwa kuwakubali maelfu ya wakimbizi kuishi nchini mwake kwa miongo miwili iliyopita.

Bi Amos atafanya mashauriano na washirika wengine kutoka mashirika mbali mbali ya Umoja wa Mataifa, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na mashirika ya kijamii kuhusu hatua zitakazo chukuliwa kukabiliana na athari za kiangazi. Baadaye Amos atasafiri kwenda nchini Somalia kuwatembelea wakimbizi wa ndani na kufanya mikutano na utawala na waakilishi wa Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali.