Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ataka kukomeshwa kwa ghasia Misri

Ban ataka kukomeshwa kwa ghasia Misri

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewataka wananchi wa Misri kujiepusha na matukio yanayoweza kuwatumbukiza kwenye umwagaji wa damu wakati huu wakiwa kwenye vugu vugu la maandano ya amani, lakini pia ameitaka serikali ya Misri kutambua kuwa hii ni fursa ya pekee ambayo inapaswa kuitumia kutanzua kero za wananchi wake.

Kupitia msemaji wake, Ban amesema kuwa Umoja wa Mataifa unafuatilia kwa karibu juu ya kile kinachoendelea nchini Misri na eneo nzima la ukanda huo, na Umoja huo utakuwa tayari kutoa msaada wowote pale itapohitajika kufanya hivyo.

Taarifa za vyombo vya habari zinasema kuwa askari wameendelea kupambana na kundi kubwa la wananchi waliomimika mitaani kufanya maandamano wakipinga mwenendo wa serikali ya Hosni Mubarak ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 30 sasa.