Skip to main content

Mawasiliano na tekinolojia kuwafaidi mamilioni:ITU

Mawasiliano na tekinolojia kuwafaidi mamilioni:ITU

Shirika la kimataifa la mawasilinao (ITU) limesema kuwa kuna hali ya kutia faraja kutokana na mapinduzi makubwa yaliyoletwa kupitia sekta ya habari, mawasilino na teknolojia ICT, ambayo sasa inawafikia mabilioni ya watu duniani kote.

Hali hiyo imefanya kuimarika kwa ustawi wa kijamii na kiuchumi jambo ambalo ITU imesema ni la kujivunia.

Akizungumza Mjini Geneva, Mkuu wa shirika hilo Hamadoun Touré,amesema kuwa sekta ya ICT katika kipindi cha miongo miwili iliyopita imeweza kupenya karibu kila pembe ya dunia na hivyo kutoa unafuu wa maisha kwa walio wengi.

Ametolea mfano kuwepo kwa watumiaji wengi wa huduma za simu za mikononi ambao sasa wanafikia zaidi ya watu bilioni 5 duniani kote.