Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo ni siku ya kumbukumbu ya mauaji ya Holocaust

Leo ni siku ya kumbukumbu ya mauaji ya Holocaust

Katika siku ya kimataifa ya kuadhimisha kumbukumbu ya mauaji ya Holocaust ambyo kila mwaka huwa Januari 27, kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa Navi Pillay amesema mauaji ya hayo yawe ni kumbusho la hatari za kuyatenga baadhi ya makundi katika jamii.

Siku hiyo ni ya kuwakumbuka mamilioni ya Wayahudi, wake kwa waume na watoto na maelfu ya waathirika wakiwemo Waroma, walemavu, wanaofanya mapenzi ya jinsia moja, mashahidi wa Jehova, Wakomunisti na wafuasi wengine wa siasa ambao maisha yao yalikatiliwa na imani za chuki na utawala wa kinazi na washirika wake.Amesema mauaji hayo yatukumbushe kwamba kauli wakati mwingine zinaweza kuigawa jamii. George Njogopa na ripoti kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)