Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali ya mpito ya Somalia lazima imalize mwezi Augusti: Mahiga

Serikali ya mpito ya Somalia lazima imalize mwezi Augusti: Mahiga

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Dr Augustine Mahiga ametangaza kwamba mkutano wa ngazi ya juu kuhusu Somalia utafanyika mjini Addis Ababa Ethiopia sambamba na ule wa muungano wa Afrika ulioanza leo.

Mkutano huo ambao umeandaliwa kwa pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na Jean Ping mwenyekiti wa tume ya muungano wa Afrika utatathimini hali ya sasa ya mchakato wa amani Somalia. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)