Ban akutana na viongozi wa Cyprus wa upande wa Uturuki na Ugiriki

Ban akutana na viongozi wa Cyprus wa upande wa Uturuki na Ugiriki

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo amekutana na viongozi wa Cyprus ya upande wa Uturuki na upande wa Ugiriki mjini Geneva.

Ajenda kubwa ya mazungumzo yao ni kutafuta njia muafaka ya kumaliza mzozo iliogawa mapande mawili kisiwa cha Cyprus.

Ban amewataka viongozi wa pande hizo mbili Demitris Christofias na Dervis Eroglu kutatua masuala muhimu yanayoghubika mzozo wao ifikapo March mwaka huu kabla ya uchaguzi wa bunge wa pande hizo mbili za kisiwa cha Cyprus.Alexander Downer ni mshauri maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Cyprus.

(SAUTI YA ALEXANDER DOWNER)